Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika kumbukumbu ya pili ya kuuawa kishahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah, Abdulilah al-Hajar, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, alirejea kuzungumzia mwenendo wa uongozi wa kiongozi aliyejitolea maisha yake yote katika jihadi na kukabiliana na uvamizi.
Alielezea nafasi yake katika kuunda muundo wa Muqawama, kuimarisha nguvu zake na kuthibitisha imani ya kwamba Muqawama una uwezo wa kufikia ushindi.
Al-Hajar anaamini kwamba: Kumbukumbu ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah imewadia katika mazingira ambayo angependa angekuwepo ili ashuhudie matunda ya mapambano na jihadi yake ya muda mrefu, pamoja na ushindi ambao Mhimili wa Muqawama umeupata; ushindi ambao yeye pamoja na Imam Shahidi, Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu), walikuwa na nafasi kubwa katika kupatikana.
Alisema: Njia hii ilijengwa juu ya imani kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Mtukufu (saww), jihadi katika njia Yake, na kutokuwa na hofu ya lawama za mwenye kulaumu. Viongozi mashahidi walianzisha Muqawama uliojengwa juu ya nguvu, imani, kumtegemea Mwenyezi Mungu na msaada wa Mwenyezi Mungu.
Aliongeza: Viongozi hawa walifikia kile walichokiamini na kukipigania, yaani kuuwawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na baada ya hapo ukatokea ushindi mkubwa pamoja na ufunguzi ulio wazi.
Al-Hajar alieleza kwamba: Mandhari ya sasa inaonesha hali ya udhaifu na kushindwa maadui wa Muqawama, pamoja na kushuka nafasi yao mbele ya dunia; iwe miongoni mwa washirika wao au miongoni mwa mataifa na nchi nyingine. Watu wengi sasa wanawaangalia maadui hao kuwa chanzo cha mateso duniani.
Sayyid Nasrullah yupo katika dhamira ya watu wa Yemen
Al-Hajar, alipokuwa akizungumzia nafasi maalumu ya Sayyid Hassan Nasrullah miongoni mwa watu wa Yemen, alisisitiza kwamba: Mapenzi yake hayakuishia kwa Walebanon au watu wa Muqawama pekee, bali yameenea kwenye mataifa ya Umma, na juu ya yote miongoni mwao ni watu wa Yemen.
Alisema: Mimi ni mmoja wa watu wa Yemen, na tunahisi kwamba mtu huyu ana fadhila na ubora juu yetu. Nafasi hii imetokana na jukumu lake katika kuuongoza Umma na kuusaidia, kusimama pamoja na mataifa ya Kiarabu na watu wa Lebanon, pamoja na kushikamana na suala la Quds, ambalo alipigania hadi alipouawa kishahidi.
Aliongeza: Sayyid Nasrullah alikuwa kiongozi wa Umma, na alikuwa na nafasi katika kufufua jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kulirejesha suala la Quds katika nafasi yake ya msingi. Sadaka na kujitolea kwake pamoja na mashahidi waliouawa kishahidi pamoja naye hakukuwa bure, bali kumeacha athari kubwa katika dhamira ya mataifa na vizazi.
Maelfu ya wapiganaji wanaiendeleza njia
Al-Hajar alisisitiza kwamba: Kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah pamoja na viongozi wengine na wapiganaji, hakukuimaliza njia ya Muqawama, bali kulisaidia katika kulea kizazi kipya kinachobeba fikra na mwenendo wao. Mashahidi hawakumjacha nyuma mtu mmoja tu mwenye sifa zao, bali wamejenga kizazi kinachoundwa na maelfu ya wapiganaji ambao katika imani, azma na utayari wa kuendelea kukabiliana, wanafanana na Sayyid Nasrullah.
Anaamini kwamba: Dunia itashuhudia, kupitia mikono ya wapiganaji hawa na pia kupitia mikono ya wana wa Umma wa Kiislamu, ushindi mkubwa katika hatua ijayo. Alieleza matumaini kwamba njia hii itasababisha kuangamizwa utawala wa Israel, ambao aliuelezea kuwa ni “saratani” katika mwili wa Umma wa Kiarabu.
Pia alieleza kwamba: Himaya ya dhuluma na uchokozi itafikia mwisho kupitia mikono ya wapiganaji, na njia hii haiishii katika upande mmoja pekee, bali wapiganaji kutoka Iran na Yemen, pamoja na maeneo mengine ya Muqawama, wanashiriki katika njia hiyo.
Al-Hajar mwishoni alisisitiza kwamba: Kumbukumbu ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah ni fursa ya kurejea katika dhana za kujitolea, kusimama imara na kufanya upya ahadi ya kuendelea na njia aliyopita.
Alisema kwamba urithi wake wa jihadi unaendelea kuwepo katika dhamira ya Umma, na akasisitiza kwamba: Vizazi vilivyokulia katika mwenendo wake vitabeba bendera hiyo na kujitahidi kuufikia ushindi.
Maoni yako